


Mgombea Urais kupitia Chama Cha mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wananchi wa Dindila atalisimamia tatizo la ardhi katika eneo hilo lililolalamikiwa kuwa ni kero ya muda mrefu na wananchi hao.
Mheshimiwa Kikwete ameyasema hayo aliposimama eneo hilo akiwa njiani kuelekea Bumbuli kwenye mkutano wa kampeni.
Alipoulizwa nini kero ya wananchi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa Kijiji alielezea kuwa ardhi ni tatizo la muda mrefu, ambapo wananchi wanaomba watengewe eneo maalumu kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Mheshimiwa Kikwete aliahidi kulivalia njuga suala hilo na huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi.
No comments:
Post a Comment