9/13/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo Mkoani Tanga

Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi leo zimeanzia Maramba wilaya ya Mkinga mkoani hapa.
Kutoka Maramba, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Wilaya ya Korogwe kupitia Daluni, Mashewa na Magoma ambapo mgombea atasalimiana na wananchi wa maeneo hayo.
Baada ya Mkutano wa Kampeni wa Korogwe, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Bumbuli kupitia Kwamsheshi, Dindira na hatimaye Bangalai ambapo pia mgombea atapata nafasi ya kusalimiana na wananchi.
Mkutano wa kampeni wa mwisho kwa siku ya leo utafanyika Lushoto. Kutokea Bumbuli kuelekea Lushoto, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utapitia Soni na kusalimiana na wananchi.

No comments:

Post a Comment