Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa Bomang'ombe kumsikiliza Mheshimiwa Kikwete alipowasili kwenye mkutano mkubwa wa kampeni.
Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na vijana wa Kwasadala ambapo aliwashangaza wengi aliposhuka na kujichanganya na wananchi wa mahali hapo.
Kabla ya kuwasili Bomang'ombe, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulisimama Kwasadala ambapo mgombea huyo alishuka na kuanza kusalimiana na wananchi waliokuwa wanamsubiri kwa shauku kubwa.
Kijana mfanyabiashara ndogondogo hapo Kwasadala alikiri kuwa hawakutegemea kumuona Mheshimiwa Kikwete na kumshika mkono, na kikubwa zaidi ni pale aliposhuka na kujichanganya na wakazi wa eneo hilo.
"Si unaona, huyu sio bishoo kabisa, ni mtu wa watu, ni mtu wa kujichanganya na huyu ndio mwenye dola. Wengine hawajashika dola lakini hawajichanganyi na sisi, ubishoo mtupu!" Alimaliza kijana huyo aliyejulikana kwa jina moja tu, Sadati.
Naye mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Fuya Kimbita alimmwagia sifa nyingi Mheshimiwa Kikwete kabla ya kuanza hotuba yake ya kampeni.
Alisema mafanikio ya wazi yamepatika Wilaya ya Hai katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hususan kwenye upande wa elimu ambapo ufaulu wa wanafunzi wa sekondari umeongezeka kutoka 42% mwaka 2005 hadi 70%. Shule mpya za Sekondary za kata 18 zimejengwa na hivyo kufanya idadi ya shule za sekiondari kufikia 43.
No comments:
Post a Comment