9/06/2010

Kampeni zasitishwa siku mbili

Kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 zimesitishwa nchi nzima kwa siku mbili kupisha mitihani ya darasa la saba inayoanza leo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Kampeni ya Mheshimiwa Kikwete, Jumatatu tarehe 6.9.2010 na Jumanne tarehe 7.9.2010 hakutakuwa na mkutano wala shughuli yoyote ya kampeni.
Kampeni hizo zitaanza tena Jumatano tarehe 8.9.2010 ambapo zitaanzia Songe, Handeni, Mkata na hatimaye Pangani Mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment