Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi amesimama Kwashemshi Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga na kulakiwa na umati mkubwa wa watu.
Mheshimiwa Kikwete alisimama Kwashemshi akitokea Korogwe kuelekea Bumbuli kwenye Mkutano wa Kampeni.
Akizungumza na wananchi hao, Mheshimiwa Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea udiwani na ubunge wa CCM.
Akimnadi Steven Ngonyani au Profesa Maji Marefu, mgombea ubunge Korogwe Vijijini Mheshimiwa Kikwete aliwaambia wananchi kwamba wamempata mtendaji na mchapakazi wampe kura zote ili ashirikiane na wengine wote wa CCM katika kuleta maendeleo.

No comments:
Post a Comment