Karibuni kwenye blogspot Jakaya Kikwete 2010. Blogspot hii ina habari za siku 70 za Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete. Blog hii haitakuwa na habari baada ya tarehe 30 Oktoba, 2010
9/08/2010
Kampeni katika picha Kilindi, Handeni
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Songe ambao ni makao makuu ya wilaya ya Kilindi wakati wa mkutano wa kampeni alioufanya wilayani humo
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,CCM, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mziha kilichoko katika wilaya ya Kilindi. Rais Kikwete yupo katika kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kibirashi kilichoko katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga akiwa katika siku ya kwanza mkoani humo ili kuomba ridhaa ya wananchi wa mkoa huo ili wawezekumchagua katika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Mheshimiwa Jakaya Kikwete, mgombea wa Urais kupitia ccm akimtambulisha Mgombea Ubunge wa jimbo la Handeni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Abdallah Kigoda wakati wa mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika mjini Handeni
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwapungia mkono mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa mkutano wa mjini Handeni kwa ajili ya mkutano wa kampeni
No comments:
Post a Comment