9/03/2010

Kampeni za Mgombea Urais CCM Zinaendelea

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na wakazi wa Mbezi baada ya kutoka kwenye kikao na viongozi wa Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni leo.
Baada ya mapumziko ya siku mbili, Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaendelea na Kampeni zake za kutetea kiti chake cha Urais.
Leo Mheshimiwa Kikwete anafanya kikao cha kazi ambapo anakutana na viongozi wa na wana CCM Wilaya ya Kinondoni kama ratiba ya kampeni inavyoelekeza.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mheshimiwa Kikwete anategemewa kufanya mikutano miwili kwenye wilaya za Kinondoni na Temeke ambapo yeye amechagua kati ya hiyo miwili mojawapo utakuwa mkutano wa ndani wa viongozi wa maeneo husika ndani ya wilaya hizo.
Akihutubia viongozi hao wa CCM, Mheshimiwa Kikwete ameeleza kwamba amechagua kutumia nafasi hii ya kufanya mkutano wa ndani na wana CCM ili kuweka mkakati wa pamoja hususan na viongozi ambao walimhakikishia Mwenyekiti wa CCM ushindi wa kishindo majimbo nane na kata 90 Wilaya ya Kinondoni.


Baadae leo Mheshimiwa Kikwete atafanya kikao na viongozi wa Jimbo la Ubungo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza na baada ya mapumziko atafanya Mkutano wa Kampeni Jimbo la Kigamboni kwenye Uwanja wa Zakhiem Mbagala.

1 comment:

  1. Watanzania tujitokeze kwa wingi kwenda kusikiliza mikutano hiyo,mana ni faraja kubwa kwa Mgombea wetu...Kila la kheri ndg Jakaya!!!

    ReplyDelete