9/17/2010

Kampeni ya Mheshimiwa Kikwete Leo

Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zimeanzia Ngaramtoni mkoa wa Arusha, ambapo atafanya mkutano wa kampeni na wananchi wa eneo hilo.
Mkutano wa pili wa kampeni kwa siku ya leo utafanyika Longido na baadaye Namanga karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania.
Baadaye leo msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Monduli na Mto wa Mbu kwa mikutano mikubwa ya kampeni na kumalizia Mbulu mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment