9/08/2010

Ratiba ya Kampeni ya Mheshimiwa Kikwete Leo

Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zimeanza tena baada ya mapumziko ya siku mbili. Kampeni hizo leo zinaanzia Kilindi, Songe.
Wakati msafara unaelekea Handeni, Mheshimiwa Kikwete atasimama kusalimiana na wananchi wa Kibirashi na Mziha.
Baada ya Mkutano wa Handeni, Mheshimiwa Kikwete atakuwa na Mkutano wa mwisho kwa siku ya leo Mkata, kabla ya kuelekea Pangani Tanga.

No comments:

Post a Comment