9/21/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo - IringaKampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mapumziko ya ziku moja leo zimeingia mkoa wa Iringa.


Mheshimiwa Kikwete aliwasili kwenye uwanja wa Nduli mjini Iringa na kupokelewa na umati mkubwa wa mashabiki na wanachama wa CCM.


Mkutano wa kwanza wa kampeni utafanyika Ilula na baada ya hapo msafara wa Mheshimiwa Kikwete utafanya mkutano wa kampeni Ismani.


Baada ya Ismani, mkutano wa kamoeni utafanyika Kalenga na Kilolo maeneo ya Boma la Ng'ombe.


Mkutano wa mwisho wa kampeni kwa siku ya leo utafanyika Iringa mjini kwenye uwanja wa Samora.

No comments:

Post a Comment