9/09/2010

Kampeni ya Mheshimiwa Kikwete Leo

Ratiba ya kampeni ya mgombea urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo tarahe 9/9/2010 imeanzia Wilaya ya Mpangani ambapo mkutano mkubwa wa kampeni ulifanyika.

Kutoka Pangani, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulivuka sehemu ya bahari kwa kutumia kivuko kipya cha MV Pangani hadi Mkwaja ambapo Mheshimiwa Kikwete alipata fursa ya kusalimiana na wananchi wa hapo.

Baada ya Mkwaja, Mheshimiwa Kikwete alihutubia mkutano wa kampeni Handeni mjini ambapo uwanja wa michezo Handeni ulifurika maelfu ya wapenzi wa CCM na wakazi wa Handeni.
Baada ya mkutano wa Handeni, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulielekea Duga kabla ya kuwasili Tanga mjini uwanja wa Mkwakwani kwa mkutano wa mwisho wa kampeni kwa siku hii ya leo.
Pangani - Mkwaja - Handeni - Duga - Mkwakwani Tanga Mjini

No comments:

Post a Comment