9/04/2010

Kampeni ya Mgombea Urais CCM - Ratiba

Ngerengere


Kampeni ya Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo imeingia Mkoa wa Morogoro. Mkutano wa Kampeni wa kwanza kwa siku ya leo utafanyika Ngerengere, Morogoro Vijijini. Baada ya hapo msafara wa Mheshimiwa Kikwete utakua Mvuha na baadae Matombo.
Kutokea Matombo msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulisimama vijiji vya Mkuyuni na Bamba ambapo mgombea wa CCM alipata nafasi ya kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wa udiwani na ubunge wa chama chake.
Msafara wa Mheshimiwa Kikwete utamalizia kampeni kwa siku ya leo Morogoro mjini ambapo umati mkubwa unamsuburia mgombea wa CCM, Mheshimiwa Kikwete.

No comments:

Post a Comment