9/22/2010

Mkutano wa Kampeni Mafinga, Wilayani Mufindi: Apokea wananchama kutoka Chadema, azawadiwa asali ya kumpa nguvu!

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na wananchi wa Mafinga mara baada ya kuwasili mahali hapo kwa mkutano wa kampeni.
Umati mkubwa wa watu wakimsikiliza Mheshimiwa Kikwete alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Mafinga, Mufindi leo mchana.
Mheshimiwa Kikwete amewasili Mafinga wilayani Mufindi na kupekelewa na wananchi wa hapo kwa zawadi za chakula na zawadi ya wanachama waliorudi Chama Cha Mapinduzi kutoka upinzani.
Akielezea zawadi hizo, Katibu wa CCM Wilaya alisema kwa niaba ya wana Mafinga, wanatambua uchuvu wa misafara ya kampeni na hivyo wamemzawadia asali ikiwa kama dawa na kirutubisho cha kumuongezea nguvu wakati akiwa safarini kunadi ilani na sera za CCM.

Kabla ya kumkaribisha Mheshimiwa Kikwete kuzungumza na umati huo mkubwa wa watu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Bwana Deo Sanga Al-maarufu kama Jah People alimkaribisha mtendaji wa CCM ili awataje wanachama wa Chadema waliorudisha kadi na kuingia CCM.

Wanachama hao wa Chadema ambao walikuwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi, walikiri kuwa sera za wapinzani hazina manufaa kwao na wameona ni dhahiri CCM ndio chama bora kwa watanzania wote bila kujali maeneo waliyotoka wala kabila.

No comments:

Post a Comment