9/14/2010

JK apokelewa kwa kishindo Ndungu aasa kuachana na vyama dhoofu wanaosubiri kushawishi wagombea walioshindwa mchakato wa CCM

Mgombea Urais CCM Mheshimiwa Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Ubunge CCM Same Mashariki Mheshimiwa Anne Kilango alipofanya mkutano wa kampeni tarafa ya Ndungu kwenye jimbo hilo.
Umati wa wana Ndungu wakimsubiri Mgombea Urais CCM awasili kwenye uwanja wa mkutano akitokea Mombo mkoani Tanga.

Mheshimiwa Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi wa Jimbo la Same Mashariki


Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokelewa kwa shangwe na umati mkubwa wa watu kwenye Jimbo la Same Mashariki wilaya ya Same tarafa ya Ndungu.

Akielezea mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM, Mbunge wa Same Mashariki Mheshimiwa Anne Kilango Malecela ameelezea kwa kuonyesha barabara ya kiwango iliyojengwa na serikali ya awamu ya nne ya CCM.

Pia amemshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kufanikisha harambee ya kuchangia ujenzi wa kiwanda cha kuwasaidia wakulima wa Tangawizi wilayani Same. Kwa niaba ya wakulima hao, Mheshimiwa Anne Kilango alimuomba Mheshimiwa kuwasaidia wataalam wa mitambo na maji pindi kiwanda hicho kitakapoanza kufanya kazi kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Naye Mgombea Urais Mheshimiwa Kikwete aliwaasa wana Ndungu kuwa makini na wanasiasa wadhoofu wanaotangaza sera za ukabila zenye nia ya kuwagawa Watanzania.

Alisema hiki ni kipindi cha uchaguzi ndio maana CCM iko makini kuhakikisha kinanadi sera makini zenye kudumisha udugu na mshikamano baina ya Watanzania. Aliongeza vyama vingine vinaibuka wakati wa uchaguzi na havina wagombea. "Wanasubiri hadi CCM imalize mchakato, waanze kuwarubuni wale walioshindwa mchakato wa ndani wa CCM, ndio wawe wagombea wao" alisema Mheshimiwa Kikwete akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Aliongeza CCM ni chama kinachoaminika na kimetizimiza ahadi zote na zaidi, ilizoahidi mwaka 2005. Mheshimiwa Kikwete alisema yeye na chama chake kimeweza kutekeleza haya yote kwa sababu kumekuwa na nia thabiti na uthubutu wa kufanya maamuzi kwa madhumuni ya kuwaendeleza Watanzania walio wengi.
Mwisho kabisa Mheshimiwa Kikwete alichukua nafasi hiyo kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa CCM, na kuwaombea kura kwa wananchi wa Ndungu ifikapo Octoba 31, 2010.

No comments:

Post a Comment