9/16/2010

Mheshimiwa Kikwete apokelewa kwa Shangwe Old Moshi KNCU asubuhi hii


Umati mkubwa wa wananchi wa Old Moshi umemlaki kwa shangwe na vigelegele Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipopita kuwasalimia kwenye eneo la Kolila KNCU kufanya mkutano wa kampeni.


Wananchi hao walimueleze Mheshimiwa Kikwete kuwa shangwe yao kwa kumuona haina mfano kwani wana deni kwa serikali ya CCM na shukrani yao kwa yaliyotekelezwa na CCM ni ujio wake mahali hapa.


Naye mgombea Urais kupitia CCM aliwaeleza wananchi hao mipango ya CCM ya kuendeleza elimu na upanuzi wa utoaji elimu Old Moshi. Alieleza shule mpya zitajengwa, vitabu vya sayansi vitatolewa bure na nyumba za walimu zitajengwa.


Mafanikio mengine yaliyoelezewa ni utoaji huduma ya afya, ujenzi wa vituo vya aafya kila kata na upanuzi wa hospitali ya mkoa KNCU.


Umati huo ulishangilia kwa kishindo Mheshimiwa Kikwete alipoelezea ujenzi wa barabara za lami mkoani Kilimanjaro.


Akielezea mpango huo mkubwa wa ujenzi wa barabara, Mheshimiwa Kikwete alisema imebaki barabara hii ya Old Moshi Kidia itakayopanda mpaka eneo la Forest.

"Tunapenda kuwahakikishia wakazi wa hapa kwamba na barabara hii pia itajengwa kwa kiwango cha lami"


Alimalizia kwa kuwanadi madiwani wa CCM na mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Cyril Chami ambaye alisema ni muadilifu na yeye anamuamini na hivyo kuwaomba wananchi wachague CCM na wagombea wake wote.

No comments:

Post a Comment