9/23/2010

Mkutano wa Kampeni Makete: JK awakosha wana Makete

Mheshimiwa Kikwete akihutubia umati mkubwa wa wana Makete kwenye mkutano wa kampeni ambapo leo umeanzia Wilayani Makete, Mkoa wa Iringa.
Mheshimiwa Kikwete akiongozana na mtoto wa Makete kwenye gari yake mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake wa kampeni leo asubuhi.

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na watoto wa Makete mara baada ya kuwasili kwa mkutano wa kampeni wilayani hapo leo asubuhi.


Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi chini ardhini kumsikiliza Mama Sara Mwageni wa Wilaya ya Makete, mara mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.


- Akanusha Minong'ono ya CCM kutojali waishio na ulemavu

- Makete wasema yeye ni mkombozi wao

- Akaa vumbini kumsabahi mlemavu

- Ana upendo wa hali ya juu kwa wana Makete, ametembelea zaidi ya mara nne

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrsiho Kikwete amewasili Makete na kupokelewa na viongozi wa chama, lakini aliyeguswa zaidi ni Mama Sara Mageni aliyelakiwa na Mheshimiwa na kufanya naye mazungumzo kwa muda.

Mama Mageni ambaye ni mlemavu wa viungo alieleza furaha yake ya kukaa chini na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa faraja sana, na katika maisha yake hakuwahi kufikiria angeweza kupata nafasi hiyo.

Akizungumzia furaha yake Mama Mageni alisema Kikwete ni mkombozi wa wana Makete nakuongeza "ni mtu wa watu, anatupenda wote sawa na anataka kila mmoja wetu kijisikia yeye ni Mtanzania na ana fursa na haki sawa" Alimalizia huku akishindwa kuficha furaha yake.
Mama Mageni alikutana na Mheshimiwa Kikwete kwenye ziara yake Makete na alimpa msaada wa Bajaj ili kurahisisha shughuli zake za kumletea kipato. Mama Mageni alisema kuonana na Mheshimiwa Kikwete tena leo ni kama amekutana na ndugu yake wa karibu wanaojuana miaka mingi.
Naye Mheshimiwa Kikwete akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, amekanusha vikali minong’ono kwamba chama chake tawala hakiwajali watu wanaoishi na ulemavu, na kusisitiza kwamba ilani ya uchaguzi ya 2005-2010 na ya 2010-2015 imeeleza kinagaubaga jinsi serikali inavyojali na kulihudumia kundi hili la wananchi.

Akiongea katika mkutano mkubwa wa kampeni Wilayani Makete leo, Mheshimiwa Kikwete pia amesema serikali yake imeridhia mkataba wa kimataifa wa kulinda na kutetea maslahi ya watu waishio na ulemavu, akiongezea kwamba utekelezaji wake utapewa kipaumbele kwenye miaka mitano ijayo.

Kumekuwepo na minong’ono kwamba watu wanaoishi na ulemavu wamekuwa wakilalamika kwa kile walichosema kutowekwa kwenye ilani za uchaguzi za vyama vinavyogombea nafasi mbalimbali, na kudai kujumuishwa kwenye mipango yote iliyopo ya kijamii na maendeleo.
Mheshimiwa Kikwete pia alitumia muda mwingi kuzungumzia suala la afya na haswa maradhi ya UKIMWI na umuhimu wa kuchagua kutukupata UKIMWI na kuchukua tahadhari. Makete ni mojawapo ya wilaya nchini Tanzania zilizoathiriwa sana na janga la UKIMWI kwa kuacha watoto wengi yatima.

Mwisho aliwanadi wagombea mbalimbali wa udiwani na ubunge na kuwasihi wana Makete wachague CCM, alisema ushindi wa kishindo wa CCM ni lazima ifikapo Oktoba mwaka huu 2010.

No comments:

Post a Comment